Kuna mambo ambayo hatuwezi kuyafumbia macho. Wakati umefika sasa Watanzania tuache siasa na unafiki tuzungumze masuala yenye tija bila kuyaonea aibu wala mas'hara.
Kuna wimbi la tabia ambalo linaenea kwa kasi sana hapa nchini-wanawake kufanya mapenzi na wanawake wenzao na wanaume halikadhalika. Hili si jambo la kulifumbia macho hata kidogo. Ingawaje tunasingizia mila na desturi zetu haziruhusu masuala kama haya, lakini yapo na yanaendelea kwa kasi kubwa siku hadi siku.
Je tatizo ni nini? Ni jamii, serikali, wahusika wenyewe au wazazi? Iwapo huko nyuma hayakuwa yakijulikana kwa kiwango hiki, kwa nini leo hii mambo yamekuwa kama yalivyo sasa? Hili ni jambo la kuniuliza na kulitafutia ufumbuzi.
Tusisingizie katiba, mila na desturi na kadhalika wa kadhalika, ukweli ni kwamba mambo yanatendeka tena kwa hadhara kabisa. Kama kweli tunataka kulinusuru taifa na vizazi vijavyo ni lazima tuzungumze, yanazungumzika, kwani mauti huumbua maradhi! Sinta (Christina Manongi) ameonyesha njia basi tufuate njia hiyo kwa nia njema kabisa. Ninaamini tutafika mahali tutazungumza lugha moja!
No comments:
Post a Comment