Sunday, February 5, 2012

Tuzungumze, yanazungumzika

Tunazungumzia mengi sana kuhusu utamaduni. Mara nyingi utamaduni huonekana kwa ubaya wake na athari zinazopatikana kutokana na kukumbatia mila mbaya na desturi zilizojengeka katika jamii. Lakini tukumbuke kwamba sio mila au tamaduni zote ni mbaya. Ziko mila ambazo zinamjenga mtu kujua asili yake, kabila lake, mila za kabila hilo, mazuri na mabaya yake. Hatuwezi kujivunia Utanzania wetu, amani na utulivu na umoja iwpo tutakuwa hatujui wapi tunatoka, mababu zetu walikuwa akina nani, kabila zetu na lugha zake na staarabu husika la kabila hilo. Utamaduni sio ngoma za asili, mavazi, chakula na kiwango cha elimu, bali ni mambo mengi kwa mapana yake yanayohusiana na kujitambua. Unajitambuaje kama Mtanzania, unajivunia nini kuwa Mtanzania na nini stara zako kama Mtanzania. Tuzungumze, yanazungumzika.

No comments:

Post a Comment